• HABARI MPYA

    Wednesday, May 04, 2016

    GUNDU GANI SIMBA! MICHUANO YA NILE BASIN NAYO YAYEYUKA

    SHIRIKISHO la Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), limeahirisha michuano ya kuwania Kombe la nchi unakopita Mto Nile ‘Nile Basin Cup’.
    Taarifa iliyotumwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicolas Musonye imesema kwamba wamepata taarifa za kuahirisha michuano hiyo kutoka kwa waratibu wakiwamo wenyeji Sudan.
    Taarifa imesema wamekubaliana kuahirisha mpaka hapo watakapotangaza tena, hivyo Simba iliyoteuliwa na TFF kushiriki michuano hiyo, imetaarifiwa kusubiri tarehe mpya ya mashindano.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GUNDU GANI SIMBA! MICHUANO YA NILE BASIN NAYO YAYEYUKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top