• HABARI MPYA

  Thursday, May 05, 2016

  STEWART HALL AAAGA AZAM FC IKIKATWA POINTI 'KIMIZENGWE'

  AZAM FC imekatwa pointi tatu na mabao matatu iliyovuna katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City Februari 20, mwaka huu Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Hiyo inafuatia madai ya kumtumia beki Erasto Edward Nyoni katika mchezo akiwa ana kadi tatu za njano.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas Mapunda amesema kwamba pamoja na kupokwa pointi hizo, benchi la Ufundi la Azam FC limepewa onyo kuwa makini na taarifa za wachezaji wake.
  Kwa kukatwa pointi hizo, Azam FC sasa inabakiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 27 na kuporomoka kwa nafasi moja hadi ya tatu, wakiipisha Simba SC yenye pointi 58 za mechi 26, huku Yanga yenye pointi 68 za mechi 27 ikiendelea kuongoza ligi hiyo.
  Katika hatua nyingine, kocha wa Azam FC Muingereza Stewart John Hall amesem ataondoka katika klabu hiyo baada ya kumaliza msimu.
  Stewart amesema anamalizia mechi tatu za Ligi Kuu na Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) na baada ya hapo ataondoka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STEWART HALL AAAGA AZAM FC IKIKATWA POINTI 'KIMIZENGWE' Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top