• HABARI MPYA

    Thursday, May 05, 2016

    FARID MUSSA AFAULU MAJARIBIO HISPANIA, DEPORTIVO TENERIFE WAJA MEZANI AZAM FC

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Farid Mussa Malik (pichani kulia) wa klabu ya Azam ya Dar es Salaam amefaulu majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Kwanza nchini Hispania.
    Mkurugenzi wa Azam FC, Yussuf Bakhresa anayefuatilia majaribio ya mchezaji huyo Hispania, ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba CD Tenerife sasa inatarajiwa kuingia katika mazungumzo na Azam FC juu ya kumnunua mchezaji huyo.
    “Tunatarajia kuanza mazungumzo nao juu ya suala la Farid, ingawa wazo lao la awali ni kumchukua kwa mkopo wa miaka miwili. Sasa tunasubiri ofa yao rasmi, kisha Bodi ya Ukurugenzi itajadili na kutoa maamuzi,”amesema Bakhresa.
    Kwa upande wake, Farid amefurahia matokeo hayo na kusema haikuwa kazi nyepesi kwake kuweza kuwaridhisha maofisa wa benchi la ufundi la Tenerife.



    “Kwa kweli nimefurahi sana na ninamshukuru Mungu kwa kufuzu majaribio, ila haikuwa kazi nyepesi, mpira wa Ulaya mgumu,”amesema.
    Awali, Farid ilikuwa apelekwe moja ya klabu za Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga, kati ya Las Palmas na Athletic ya Bilbao kwa majaribio, lakini wakala wake akashauri mchezaji huyo aanzie timu ya Daraja la Kwanza Hispania ili kupata nafasi ya kucheza na kuinuka haraka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FARID MUSSA AFAULU MAJARIBIO HISPANIA, DEPORTIVO TENERIFE WAJA MEZANI AZAM FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top