• HABARI MPYA

  Wednesday, May 04, 2016

  MWEKA HAZINA WA ZAMANI WA CAF AFARIKI DUNIA

  MWEKA Hazina wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Gamal Taha (pichani kushoto) amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 71.
  Taarifa ya Rais wa CAF, Issa Hayatou kwa BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE, imesema kwamba Gamal alikuwa zaidi ya Mhasibu ndani ya shirikisho hilo.
  "Gamal hakuwa tu Mhasibu wa CAF, bali pia alikuwa kiongozi mzuri ambaye alijenga misingi ya CAF kuwa taasisi inayojiendesha kisomi,"amesema Hayatou.
  Akiwa anafahamika kwa jina la ‘Bw Gamal’ tu mbele ya wengi, amefariki Jumatatu Mei 2 baada ya kuugua kwa muda mfupi nchini kwao, Misri.
  Alistaafu kazi CAF mwaka 2013, akihitimisha miongo miwili ya kufanya kazi za soka ya bara la Afrika alizoanza Januari mwaka 1992. Gamal ameacha mke na watoto watatu, akiwemo wa kiume Ahmed, ambaye sasa ni mfanyakazi wa CAF pia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWEKA HAZINA WA ZAMANI WA CAF AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top