• HABARI MPYA

  Wednesday, May 04, 2016

  'MKWASA WA ETHIOPIA' ATUPIWA VIRAGO VYAKE

  SHIRIKISHO la Soka Ethiopia (EFF) limeachana na kocha wake, Yohannes Sahle (pichani kulia) mwaka mmoja kabla hajamaliza Mkataba wake.
  Hatua hiyo inafuatia matokeo yasiyoridhisha ya  Walia Antelopes huuu katika mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017, ambako wamepoteza matumaini ya kufuzu kwa fainali hizo nchini Gabon.
  "Mkataba ambao ulisainiwa Mei 1, 2015, baina ya kocha Sahle na Shirikisho umevunjwa Mei 2, 2016," imesema taarifa ya EFF.
  Sahle alichukua nafasi ya Mreno, Mariano Barreto Aprili mwaka 2015, lakini ameondolewa kutokana na matokeo mabaya mechi za kufuzu AFCON na Kombe la Dunia.
  Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa, amejikuta katika wakati mgumu baada ya Ethiopia kufungwa 7-1 na Algeria Machi mwaka huu. 
  Kocha huyo mwenye umri wa miaka 49 aliiongoza Ethiopia kwenye fainali ya Kombe la  CHAN nchini Rwanda mapema mwaka huu, ambako Walia walitolewa bila kushinda hata mechi moja ya kundi lake.
  Walia wakashika nafasi ya tatu kwenye CECAFA Challenge nyumbani mwezi Desemba mwaka jana. Kocha Msaidizi, Fasil Tekalegn na kocha wa makipa, Ali Redi pia wameondolewa kwenye benchi la Ufundi. 
  Wakati huo huo, Shirikisho linatarajiwa kumtaja kocha mpya kwa ajili ya mchezo ujao wa kufuzu AFCON dhidi ya Lesotho mwezi Juni. 
  Ethiopia ina pointi tano katika Kundi J nyuma ya vinara Algeria wenye pointi 10 na lazima washinde dhidi ya Lesotho na Shelisheli Septemba ili kujaribu kufuzu kama kama mmoja wa washindi wa pili bora.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 'MKWASA WA ETHIOPIA' ATUPIWA VIRAGO VYAKE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top