• HABARI MPYA

    Thursday, May 05, 2016

    MCHAKATO WA MAREKEBISHO YA KANUNI LIGI KUU WAANZA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    BODI ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeziomba klabu kuwasilisha maoni kwa ajili ya marekebisho ya kanuni za ligi hiyo.
    Bodi hiyo pamoja na kuzipongeza timu za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kushiriki na kufanya msimu wa Ligi Kuu Bara kuwa ya Vodacom 2015/16 kuwa wenye mafanikio, imezifahamisha klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/17 juu ya mchakato wa wa utengenezaji kanuni umeanza.
    "Bodi ya Ligi kwa sasa inakaribisha maoni, mapendekezo, marekebisho kutoka klabu ili kuboresha uendeshaji wa ligi. Maoni hayo yanapokelewa kwa njia ya maandishi moja kwa moja kwenye ofisi za bodi au kwa njia ya barua pepe tplb.tplb@yahoo.com,"imesema taarifa ya Bodi kupitia TFF (Shirikisho la Soka Tanznaia).

    Katika hatua nyingine, timu ya Azam FC ya Dar es Salaam, imenyang'anywa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu uliyoupata katika mechi Na. 156 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City.
    Uamuzi huo umetokana na Azam kumtumia mchezaji Erasto Nyoni kwenye mechi hiyo wakati akiwa na kadi tatu za njano. Mchezo huo ulifanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
    Kitendo hicho ni kinyume na Kanuni ya 37(4) ya Ligi Kuu Toleo la 2015 inayoelekeza kuwa mchezaji atakayeonywa kwa kadi ya njano katika michezo mitatu hataruhusiwa kucheza mchezo unaofuata wa timu yake. Hivyo kwenda kinyume na Kanuni husika.
    Kwa kuzingatia Kanuni ya 14(37) ya Ligi Kuu Toleo la 2015, timu ya Mbeya City imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu.
    Kadhalika Bodi ya Ligi imelionya Benchi la Ufundi la timu hiyo kuongeza umakini katika utunzaji wa kumbukumbu za kadi za wachezaji wake. Pia imezikaribisha timu zote wakati wowote kuomba kumbukumbu zozote kila zinapozihitajika. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MCHAKATO WA MAREKEBISHO YA KANUNI LIGI KUU WAANZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top