• HABARI MPYA

  Wednesday, May 11, 2016

  HAJIB ABADILISHIWA TIMU TENA SAUZI SASA KUJARIBIWA GOLDEN ARROWS

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Ibrahim Hajib sasa atafanyiwa majaribio katika klabu ya Lamontville Golden Arrows F.C. ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
  Meneja wa mchezaji huyo, Juma Ndabila ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba wakala wao nchini humo, Rodgers ndiye ameamua Hajib aanzie Arrows yenye maskani yake Durban pia.
  Awali, Hajib ilikuwa kesho aanze majaribio klabu nyingine ya Ligi Kuu nchini humo, AmaZulu ya Durban pia.
  Hajib na Ndabile wapo Durban tangu Jumatatu baada ya kuwasili wakitokea Dar es Salaam.
  Hajib (kushoto) akiwa na wakala wake, Rodgers mjini Durban leo

  Hajib aliondoka nchini asubuhi ya jumatatu, ikiwa ni siku moja tangu atolewe kwa kadi nyekundu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara timu yake, Simba ikilala 1-0 mbele ya Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Taifa, Jumapili.
  Na kwa sababu kwa kadi Hajib asingeweza kucheza mechi mbili kati ya tatu za mwisho za Simba, akaona ni wakati mwafaka kutimiza mpango wake wa kwenda kujaribu bahati yake sehemu nyingine. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAJIB ABADILISHIWA TIMU TENA SAUZI SASA KUJARIBIWA GOLDEN ARROWS Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top