TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na winga, Zidane Ally Sereri mawili akiiadhibu timu yake ya zamani dakika ya tano na 71 na kiungo Feisal Salum Abdallah dakika ya 12.
Kwa ushidi huo, Azam FC inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 13 na kurejea nafasi ya tatu ikiizidi tu wastani wa mabao Simba SC ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Dodoma Jiji FC baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 21 za mechi 17 sasa wakishuka kwa nafasi moja hadi ya saba.



.png)
0 comments:
Post a Comment