• HABARI MPYA

    Friday, March 13, 2026

    FOUNTAIN GATE YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO, SARE 1-1 NA MASHUJAA KIGOMA

    TIMU ya Mashujaa FC imelazimishwa sare ya kudungana bao 1-1 na Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni hii Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
    Beki Nyenyezi Shaaban alianza kuifungia Mashujaa FC dakika ya 55, kabla ya Sadick Ramadhani ‘Immobile’  kuisawazishia Fountain Gate dakika ya 90’+4.
    Kwa matokeo hayo, Mashujaa FC inafikisha pointi 18, ingawa inabaki nafasi ya 11 ikiizidi pointi mbili Fountain Gate baada ya timu zote kucheza mechi 16 hadi sasa.
    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FOUNTAIN GATE YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO, SARE 1-1 NA MASHUJAA KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top