• HABARI MPYA

    Thursday, March 12, 2026

    DEPU ATOKEA BENCHI KUIFUNGIA YANGA BAO MUHIMU LA USHINDI


    BAO la dakika ya 78 la mshambuliaji Muangola, Laurindo Dilson Maria Aurelio ‘Depu’ limewasaidia mabingwa watetezi, Yanga SC kushinda 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
    Depu aliyeingia uwanjani dakika ya 61 kuchukua nafasi ya kiungo Mohamed Damaro Camara alifunga bao hilo akimalizia mpira uliopanguliwa na kipa Mussa Mbisa kufuatia mpira wa adhabu wa winga Mganda, Allan Okello.
    Kwa ushindi huo, Yanga SC wanafikisha pointi 35 katika mchezo wa 13 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, wakifuatiwa na JKT Tanzania yenye pointi 28 za mechi 17, Azam FC pointi 27 za mechi 13 na Simba SC pointi 27 za mechi 12.
    Hali inazidi kuwa mbaya kwa Tanzania Prisons baada ya kupoteza mchezo wa leo, ikibaki na pointi zake 13 katika nafasi ya 15 mbele ya KMC inayoshika mkia kwa pointi zake nane kwenye ligi ya timu 16 baada ya wote kucheza mechi 16
    Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu.
    Timu itakayofungwa itakwenda kumenyana na timu kutoka Ligi ya Championship katika mechi nyingine mbili za mchujo nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla ndiye atacheza Ligi Kuu msimu ujao.    

    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DEPU ATOKEA BENCHI KUIFUNGIA YANGA BAO MUHIMU LA USHINDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top