• HABARI MPYA

    Tuesday, May 10, 2016

    GEBERMEDHIN HAILE NDIYE KOCHA MPYA WA ETHIOPIA

    SHIRIKISHO la Soka Ethiopia (EFF) limeteua Gebermedhin Haile (pichani kushoto) kukaimu ukocha wa timu ya taifa kwa muda. 
    Kamati ya Utendaji ya EFF imeamua kumteua Haile, ambaye anafundisha timu ya Jeshi la nchi hiyo kuwa kocha wa Walias kwa makubaliano ya muda mfupi. 
    “Shirikisho limesaini Mkataba wa muda mfupi na kocha Gebremedhin Haile. Mkataba huo utaanza Mei 9, 2016 hadi Oktoba 9, mwaka 2016,” taarifa ya EFF imesema. 
    Haile anakabiliwa na jukumu la kushinda mechi mbili zilizobaki za kufuzu AFCON mwaka 2017. Ethiopia itasafiri hadi Maseru kucheza na Lesotho mwezi Juni kabla ya kuhitimisha kampeni zake kwa kumenyana na Shelishelei Septemba.
    Haile anachukua nafasi ya Yohannes Sahle ambaye Mkataba wake ulivunjwa wiki chache zilizopita kutokana na matokeo mabaya. 
    Haile, mshambuliaji hatari enzi zake anacheza timu ya taifa ya Ethiopia na aliyewahi amefundisha timu za nyumbani kwao kwa mafanikio zikiwemo Trans Ethiopia, Ethiopian Insurance, Ethiopian Coffee na Dedebit. 
    Alikuwa kocha Msaidizi wakati Ethiopia inatwaa ubingwa wa CECAFA Challenge mwaka 2004, na tayari ameiwezesha Defence Force kutwaa mataji mawili ya Kombe la Ethiopian. 
    Jukumu lake la kwanza litakuwa ni mchezo wa kufuzu AFCON 2017 dhidi ya Lesotho Juni. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GEBERMEDHIN HAILE NDIYE KOCHA MPYA WA ETHIOPIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top