• HABARI MPYA

  Thursday, May 05, 2016

  BEKI YANGA AKARIBIA KUSAINI BONGE LA DILI ‘MAJUU’

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI aliyecheza Yanga kwa muda mfupi mwaka jana, Mghana Joseph ‘Teteh’ Zuttah yuko mbioni kusajiliwa na ZweKapin United FC yenye maskani yake Burmese, Hpa-An, Myanmar. 
  Na anayekaribia kufanikisha mpango wa Zuttah kusajiliwa na timu hiyo ya Ligi Kuu ya Myanmar ni wakala maarufu wa wachezaji, Gibby Kalule raia wa Uganda.
  Gibby amesema alivutiwa na Zuttah alipokutana naye Tanzania na baada ya kuachwa Yanga akaamua kumuingiza katika orodha ya wachezaji wake wa kuwatafutia timu.
  Joseph Zuttah (katikati) akiwa mazoeizini kwenye majaribio Myanmar
  Joseph Zuttah (kushoto) akiwa na Gibby Kalule wakipata chakula hoteli 

  “Nipo na Zutah hapa (Myanmar) alikuja kwa majaribio na amefanya vizuri, anakaribia kusaini Mkataba ambao atalipwa mshahara wa dola (za Kimarekani 7,000),”amesema Gibby akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE jana.    
  Zuttah aliyezaliwa Agosti 22, mwaka 1994, alitua Yanga Julai mwaka jana akitokea klabu ya Medeama ya kwao, lakini akaachwa baada ya mechi saba ndani ya mwezi mmoja.
  Na Zuttah alikuwa chaguo la kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van der Pluijm aliyemuona mchezaji huyo wakati anafundisha Ghana.
  Gibby (kushoto) akiwa na mchezaji mwingine Mbrazil (anayemfuatia) ambaye amefanikiwa kumuuza Myanmar 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI YANGA AKARIBIA KUSAINI BONGE LA DILI ‘MAJUU’ Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top