• HABARI MPYA

  Thursday, April 07, 2016

  YANGA YASAKA MILIONI 220 IKAIMALIZE AL AHLY CAIRO

  VIINGILIO YANGA V AL AHLY:
  VIP A: Sh 30, 000
  VIP B: Sh 25, 000
  VIP C: Sh 25, 000
  Mzunguko: Sh 5,000
  (Mchezo utaanza Saa 10:00 jioni Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam)
  Simon Msuva atapata nafasi ya kucheza dhidi ya Al Ahly kwa mara ya pili? 

  YANGA inahitaji Sh. Milioni 220 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly nchini Misri Aprili 19.
  Yanga watakuwa wenyeji wa Ahly Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya timu hizo kurudiana Aprili 19 mjini Cairo.
  Na leo Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro amewaambia Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba wanapaswa kudhibiti mapato ya mchezo wa kwanza Jumamosi ili wapate fedha za maandalizi ya mchezo wa marudiano. 
  Amesema fedha hizo zitapatikana kwa kudhibiti mapato ya milangoni, ikiwemo kuzuia kituo chochote cha Televisheni kuonyesha mchezo huo bila makubaliano maalumu.
  "Kuna baadhi ya vituo vya Televisheni vya nje vimeomba kurusha matangazo ya mchezo
  huo, tuko katika mazungumzo nao, tukikubaliana watarusha,"alisema Muro.
  Ameweka wazi kwa hapa nchini hakuna kituo chochote cha Televisheni kitakachoruhusiwa kurusha mchezo huo, zaidi ya vituo vya Redio tu kutangaza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YASAKA MILIONI 220 IKAIMALIZE AL AHLY CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top