• HABARI MPYA

    Sunday, February 01, 2026

    SINGIDA BLACK STARS PUNGUFU YACHAPWA 2-1 KONGO


    WENYEJI, AS Otohô wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa Kundi C Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa Alphonse Massemba-Débat Jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo.
    Mabao yote ya Association Sportive Otohô yenye maskani yake mjini Oyo yamefungwa na mshambuliaji chipukizi wa miaka 22,  Pomi Sagesse Exaucé Nzaou dakika ya 52 na 80, huku bao pekee la Singida Black Stars likifungwa na mshambuliaji Muivory Coast, Joseph Guédé Gnadou dakika ya 90.
    Singida Black Stars ilipata pigo la mapema kufuatia kipa wake, Metacha Borniphace Mnata kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 27‎.
    Kwa matokeo hayo, AS Otohô inafikisha pointi sita na kusogea nafasi ya pili nyuma ya CR Belouizdad yenye pointi tisa, wakati Singida Black Stars inabaki na pointi zake nne sawa na Stellenbosch ya Afrika Kusini kufuatia timu zote kucheza mechi nne.
    Mchezo mwingine wa Kundi C leo CR Belouizdad imeitandika Stellenbosch 3-0 Uwanja wa Athlone Jijini Cape Town, Afrika Kusini.
    Mechi zijazo Singida Black Stars wataikaribisha CR Belouizdad Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar na 
    AS Otohô wataikaribisha Stellenbosch hapo hapo Uwanja wa Alphonse Massemba-Débat Jijini Brazzaville.


    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SINGIDA BLACK STARS PUNGUFU YACHAPWA 2-1 KONGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top