• HABARI MPYA

  Thursday, April 07, 2016

  SIMBA SC: HAKUNA MCHEZAJI ANAYEDAI MSHAHARA, KIIZA NA JUUKO WANA YAO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 
  SIMBA SC imesema hakuna mchezaji wa klabu hiyo anayedai mshahara na kwamba kuchelewa kwa Waganda Juuko Murshid na Hamisi Kiiza kunatokana na sababu zao wenyewe binafsi.
  Akizungumzia na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Ofisa Habari w Simba SC, Hajji Manara amesema kwamba Juuko na Kiiza wamechelewa kwa matatizo yao, lakini si suala la kudai mishahara.
  “Hakuna mchezaji anayeidai Simba mshahara, wote wamelipwa, hawa wamechelewa kwa matatizo yao,"amesema Manara.
  Juuko Murshid (kulia) amechelewa kurejea Simba baada ya ruhusa

  Hata hivyo, pamoja na klabu kusema itawaandikia barua ya onyo, lakini Manara amesema wawili hao wanatarajia kuripoti kambini leo, kujiunga na wenzao kwa maandalizi ya mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya Coastal Union Aprili 11.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC: HAKUNA MCHEZAJI ANAYEDAI MSHAHARA, KIIZA NA JUUKO WANA YAO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top