• HABARI MPYA

    Saturday, April 23, 2016

    YANGA ‘YAMTIA PINGU’ JUMA ABDUL HADI 2018

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    BEKI hodari wa kulia wa kimataifa wa Tanzania, Juma Abdul Jaffar Mnyamani amesaini Mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga SC ya Dar es Salaam hadi mwaka 2018.
    Habari kutoka ndani ya Yanga ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE imezipata zinasema kwamba Abdul alisaini Mkataba huo kabla ya timu hiyo kwenda Misri kucheza na Ahly.
    Na hakuna kingine kilichoisukuma Yanga kumsainisha Mkataba mpya beki wake huyo zaidi ya kiwango chake kizuri kwa sasa akionekana kabisa kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu kikosini.
    Juma Abdul (kushoto) amesaini Mkataba utakaomuweka Jangwani hadi 2018 

    Na kwa kusaini Mkataba huo, Juma ataingia kwenye orodha ya wachezaji walioitumikia klabu hiyo kwa muda mrefu.
    Juma aliyezaliwa Novemba 10, mwaka 1992
    Mwananyamala, Dar es Salaam, alijiunga na Yanga mwaka 2012 akitokea Mtibwa Sugar kwa Mkataba wa miaka miwili, ambao ulipoisha akaongezwa mwingine wa miaka miwili.
    Na wakati Mkataba wake wa sasa unaelekea kumalizika mwishoni mwa msimu, inaelezwa tayari Juma Abdul amesaini Mkataba mwingine mpya wa miaka miwili utakaomfanya afikishe miaka sita Jangwani.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA ‘YAMTIA PINGU’ JUMA ABDUL HADI 2018 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top