• HABARI MPYA

    Saturday, April 23, 2016

    LIGI NDOGO BARA KUANZA MEI 11, LIGI YA MABINGWA WA MIKOA NAYO...

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KAMATI ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetangaza kuanza kwa ligi ndogo Mei 11, 2016 katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam itakayozishirikisha jumla ya timu nne.
    Timu zilishoshika nafasi ya pili katika msimamo wa SDL kwa kila kundi, Abajalo FC (Dar es salaam), Pamba FC (Mwanza), Mvuvumwa (Kigoma), Mighty Elephant (Songea) zitacheza ligi hiyo kusaka timu mbili zitakazoungana na timu nne za juu kupanda ligi daraja la kwanza (FDL) msimu ujao.
    Klabu nne za Allicane Schools (Mwanza), Mshikamano FC (Dar es salaam), Mbeya Warriors (Mbeya) na Singida United (Singida) zilizoongoza msimamo wa makundi ya SDL zitaungana na timu mbili kupanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.

    Wakati huo huo: TFF imetangaza Mei 14, 2016 kuwa tarehe ya kuanza kwa Ligi ya Mabingwa wa mikoa (RCL) itakayozishirkisha bingwa wa kila mkoa kutoka katika mikoa 27 nchini.
    Ligi hiyo ya mabingwa wa mikoa itachezwa katika vituo vine nchini, ambapo mshindi wa kila kundi atapanda moja kwa moja ligi daraja la pili (SDL) na mshindi wa pili mwenye matokeo mazuri kutoka kundi A, B na C.
    Kundi A kituo cha (Njombe) kutakua na mabingwa wa mikoa ya Ruvuma, Iringa, Mbeya, Rukwa, Katavi, Dar es salaam 3, Morogoro, Kundi B kituo cha (Morogoro) kitakua na mabingwa wa mikoa ya Pwani, Mtwara, Lindi, Dar es salaam 1, Dar es salaam 2, Tanga, na Singida.
    Kundi C kituo cha (Singida) kitakua na mabingwa wa mikoa ya Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Tabora, Kagera, Manyara, na Njombe, huku kundi D kituo cha (Kagera) kikiwa mabingwa wa mikao ya Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara na Kigoma.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LIGI NDOGO BARA KUANZA MEI 11, LIGI YA MABINGWA WA MIKOA NAYO... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top