• HABARI MPYA

    Friday, April 29, 2016

    COSAFA 2016; WATETEZI NAMIBIA WAPEWA BOTSWANA ROBO FAINALI

    RAUNDI YA KWANZA KOMBE LA COSAFA CASTLE...
    Kundi A
    A1 – Zimbabwe
    A2 – Swaziland
    A3 – Seychelles
    A4 – Madagascar
    Kundi B
    B1 – Malawi
    B2 – Angola
    B3 – Lesotho
    B4 – Mauritius 
    ROBO FAINALI
    1 – Afrika Kusini Vs Mshindi Kundi B
    2 – Botswana Vs Namibia
    3 – Zambia Vs Mshindi Kundi A
    4 – DRC Vs Msumbiji
    Namibia ni wenyeji na mabingwa watetezi, ambao wataanza kutetea taji dhidi ya Botswana 

    MABINGWA watetezi wa Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA), Namibia wataanza kutetea taji lao dhidi ya Botswana katika Robo Fainali.
    Katika droo ya michuano hiyo inayoanza Juni 11 hadi 25 mwaka huu nchini Namibia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wataanza na washindi wa pili wa mwaka jana, Msumbiji, wakati Zambia na Afrika Kusini watakutana na washindi wa kwanza wa makundi A na B.
    Makundi hayo yana timu tishio ambazo ni Zimbabwe, Swaziland, Shelisheli na Madagascar zilizo Kundi A, wakati Kundi B kuna Malawi, Angola, Lesotho na Mauritius.
    Mechi za Raundi ya kwanza za makundi zitachezwa Juni 11, huku mshindi wa kila kundi akienda Robo Fainali.
    Michuano hiyo itaendelea kwa hatua ya mtoano, huku timu zitakazofungwa katika Robo Fainali zikiangukia katika michuano ya Plate, ambayo ilianza mwaka 2013 na bingwa wa mwaka jana ni Malawi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COSAFA 2016; WATETEZI NAMIBIA WAPEWA BOTSWANA ROBO FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top