• HABARI MPYA

    Tuesday, April 26, 2016

    YANGA WATOA YA MOYONI KILICHOTOKEA MKWAKWANI, WATAKA COASTAL IADHIBIWE

    Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
    UONGOZI wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam umesema umesikitishwa na matukio ya uvunjwaji wa amani yaliyofanywa kwa makusudi mashabiki wa Coastal Union Aprili 24, 2016 katika mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) Uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
    Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit amesema kwamba kitendo cha mashabiki kumpiga mawe mwamuzi wa pembeni na kumjeruhi, kamwe hakiwezi kuvumilika katika mchezo wa mpira wa miguu unaotawalia na kauli mbiu ya "fair play".
    Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit (kushoto) akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ayoub Nyenzi (kulia) jjuzi Uwanja wa Mkwakwani, Tanga
    Viungo Thabani Kamusoko wa Yanga (kushoto) na Dk. Ayoub Yahya (kulia) wakigombea mpira katika mchezo huo

    “Kwetu sisi Yanga, hiki ni  kitendo cha kufedhehesha sana, pale mchezo ambao hutumika kama burudani na ukiwa unaongozwa na sheria unapogeuzwa kuwa mchezo wa vurugu na uvunjwaji wa sharia,”. 
    Uongozi wa Yanga una imani kubwa na  taasisi husika kuwa zitawachukulia hatua za kisheria na kinidhamu wale wote waliohusika katika vurugu zilizotokea, ili iwe fundisho kwa watu wote wenye tabia zisizo za kimpira,”.
    maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup kati ya wenyeji, Coastal Union na Yanga na Dar e Salaam zimetua TFF.
    Mchezo huo ulivunjika dakika ya 110 wakati Yanga ikiwa mbele kwa mabao 2-1 kufuatia mshika kibendera namba mbili, Charles Simon kupasuliwa juu ya jicho la kushoto kwa jiwe lililotupwa na shabiki.
    Coastal Union ilitangulia kwa bao la kiungo Mcameroon, Youssouf Sabo kabla ya Yanga kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma, mabao yote kipindi cha pili.
    Mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe akaifungia Yanga bao la pili mwanzoni tu mwa dakika 30 za nyongeza baada ya dakika 90 kumalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1.
    Baada ya bao hilo, mchezo ukasimama dakika ya 105 kufuatia mashabiki wanaodaiwa kuwa ni wa Coastal kuanza kutupa chupa na mawe uwanjani na kumjeruhi mshika kibendera namba mbili, Charles Simon juu ya jicho la kushoto. 
    Refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga akapuliza kipyenga cha kuhitimisha mchezo huo dakika ya 110, huku mashabiki wakiendelea kuushambulia uwanja kwa mawe na chupa.
    Kamisaa wa mechi, Osuri Kosuri kutoka Simiyu alisema kuwa wamelazikika kuvunja mchezo kufuatia vurugu zilizotokea uwanjani. 
    Kosuri alisema kuwa Usalama ulikuwa mdogo uwanjani hapo na askari walishindwa kuhimili vurugu. 
    Iwapo Yanga itapewa ushindi, itamenyana na Azam FC katika fainali mwezi ujao. Azam jana iliitoa Mwadui FC kwa penalti 5-3 kufuatia sare ya 2-2 baada ya dakika 120 Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA WATOA YA MOYONI KILICHOTOKEA MKWAKWANI, WATAKA COASTAL IADHIBIWE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top