• HABARI MPYA

    Saturday, April 23, 2016

    MWANZA WAULA, WAPATA TIMU YA PILI LIGI KUU, NI MBAO FC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KWA mara ya kwanza baada ya miaka mingi, msimu ujao Mwanza inaweza kuwa na timu mbili katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Hiyo inafuatia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeitangaza klabu ya Mbao FC ya mjini Mwanza kupanda Ligi Kuu kutoka katika kundi C la Ligi Daraja la Kwanza. Mbao sasa itaungana na Toto Africans msimu ujao.
    TFF imeitangaza Mbao FC kfuatia maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF yaliyotolewa April, 2016 ya kuzishusha daraja timu nne kutoka kundi C baada ya kukutwa na hatia ya upangaji matokeo.
    Mbao FC imeshika nafasi ya kwanza kundi C kwa kuwa na pointi 12 baada ya kufutwa kwa matokeo ya timu za Geita Gold, Polisi Tabora, JKT Oljoro na JKT Kanembwa zilizokumbwa na mkasa huo wa upangaji matokeo.

    Timu ya Mbao FC inapanda ligi kuu (VPL) msimu ujao, sambamba na timu za African Lyon ya jijini Dar es salaam pamoja na Ruvu Shooting ya mkoa wa Pwani.
    Wakati huo huo kikao cha Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF kinatarajiwa kukaa Jumamosi ijayo April, 30 jijini Dar es salaam kujadili rufaa mbalimbali ambazo zimekatwa na kutokana na maamuzi ya kamati ya Nidhamu ya TFF.
    Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya TFF itasikiliza rufaa za wafuatao waliokata rufaa, ambao ni Saleh Mang’ola, Yusuph Kitumbo, Amos Mwita, Fateh Remtullah na timu za JKT Oljoro na Polisi Tabora.
    Aidha Kamati ya Nidhamu ya TFF itakutana Jumapili Mei Mosi kupitia taarifa mbalimbali zilizowasiliswa katika kamati hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWANZA WAULA, WAPATA TIMU YA PILI LIGI KUU, NI MBAO FC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top