• HABARI MPYA

    Thursday, April 21, 2016

    YANGA ITAPEWA TIMU IPI KATI YA HIZI NANE?

    ZILIZOFUZU NANE BORA LIGI YA MABINGWA;
    Enyimba (Nigeria), Al Ahly (Misri), AS Vita (DRC), Asec Mimosas (Ivory Coast), Wydad Casablanca (Morocco), ES Setif (Algeria), Zamalek (Misri) na
    Zesco United (Zambia).
    ZILIZOANGUKIA KOMBE LA SHIRIKISHO;
    ES Sahel (Tunisia), Yanga SC (Tanzania), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Ahly Tripoli (Libya), TP Mazembe (DRC), El Merreikh (Sudan), MO Bejaia (Algeria) na Stade Malien (Mali).
    ZILIZOFUZU KOMBE LA SHIRIKISHO;
    Kawkab Marrakech (Morocco), Mounana (Gabon), Misr Makkassa (Morocco), Medeama (Ghana), FAR Rabat (Morocco), Esperance (Tunisia), Sagrada Esperanca (Angola) na Stade Gabesien (Tunisia).

    Na Prince Akbar, ALEXANDRIA
    YANGA SC inaweza kurudishwa Kaskazini mwa Afrika kwa ajili ya mchezo wa kuwania kuingia kwenye makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika.
    Yanga jana ilitolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1 na Al Ahly Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora.
    Al Ahly imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kulazimisha sare ya 1-1 Uwanja wa Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.
    Abdallah Said aliifungia Ahly bao la ushindi dakika ya sita ya muda wa nyongeza baada ya kukamilika kwa dakika 90 za kawaida za mchezo akimalizia krosi ya  Walid Soliman kutoka upande wa kushoto.
    Al Ahly walitangulia kupata bao katika mchezo wa leo kupitia kwa kiungo Hossam Ghaly aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Ahmed Fathi dakika ya 52.
    Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma akaisawazishia Yanga dakika ya 57 kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya beki wa kulia Juma Abdul.
    Kwa matokeo hayo, Yanga itamenyana na moja ya timu zilizofuzu Kombe la Shirikisho kuwania nafasi ya kupangwa kwenye makundi.
    Na kati ya timu hizo nane, tano zinatoka Kaskazini mwa Afrika, ambazo ni Kawkab Marrakech, Misr Makkassa, FAR Rabat zote za Morocco, Esperance na Stade Gabesien za Tunisia.
    Timu nyingine zilizofuzu hatua hiyo ni CF Mounana ya Gabon, Medeama ya Ghana na Sagrada Esperanca ya Angola.
    Mbali na Yanga, timu nyingine zilizoangukia kwenye kapu la kuwania hatua ya makundi Kombe la Shirikisho ni pamoja na waliokuwa mabingwa wa Afrika, TP Mazembe ya DRC, Etoile du Sahel ya Tunisia, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Al Ahly Tripoli ya Libya, El Merreikh ya Sudan, MO Bejaia ya Algeria na Stade Malien ya Mali.
    Kwa Yanga, hii ni mara ya pili kufikia hatua hiyo baada ya mwaka 2007. Mwaka huo Yanga ilifungwa 3-0 na Esperance ya Tunisia katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kutoa sare 0-0 Mwanza.
    Katika kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho na ilitolewa na El Merreikh ya Sudan, ikitoa sare ya 0-0 Mwanza na kufungwa 2-0 Khartoum.
    Droo ya mchujo wa mechi za kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho inatarajiwa kupangwa mchana wa leo mjini Cairo, Misri. Je, safari hii Yanga itapangwa na nani? 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA ITAPEWA TIMU IPI KATI YA HIZI NANE? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top