• HABARI MPYA

    Monday, April 25, 2016

    MAHREZ NDIYE MWANASOKA BORA WA MWAKA LIGI KUU ENGLAND

    WASHINDI WA TUZO ZA PFA 2016

    Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA: Riyad Mahrez  
    Mchezaji Bora wa Kike wa Mwaka wa PFA: Izzy Christiansen
    Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa kike wa PFA: Beth Mead
    MSHAMBULIAJI wa Leicester City, Riyad Mahrez usiku wa kuamkia leo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA) katika Ligi Kuu ya England.
    Mahrez amekuwa na msimu mzuri kwa vinara hao wa Ligi Kuu ya England- hadi sasa akiwa amefunga mabao 17 na kuseti 11.
    Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Algeria, ambaye amekuwa chachu ya mafanikio kwa mabingwa hao watarajiwa England, alikabidhiwa tuzo yake katika ukumbi wa hoteli ya Grosvenor Hotel mjini London na kuwashukuru wachezaji wenzake.
    "Sifa zote zinakwenda kwao, kabisa, na kwa kocha na benchi la ufundi. Bila wao nisingepokea tuzo hii na nisingefunga. Ni hamasa ya timu, na ninataka kuilekeza kwao," amesema Mahrez akiwashukuru wachezaji wenzake wa Leicester kwa mafanikio yake.
    Mahrez amekuwa na mchango mkubwa kwa timu yake na sasa anaungana na washindi wa awali wa tuzo hiyo wakiwemo Kenny Dalglish, Dennis Bergkamp, Thierry Henry, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale.
    Kikosi cha Claudio Ranieri kinahitaji angalau pointi tano katika mechi zake tatu zilizobaki ili kutawazwa kuwa mabingwa wapya wa England kwa mara ya kwanza katika historia yao.
    Mahrez pia alifunga katika mchezo wa Ligi Kuu usikubwa jana Uwanja wa King Power, Leicester wakiitandika Swansea 4-0 kabla ya kukumbizwa kwenye sherehe za tuzo kwa helikopta baada ya mechi.
    Mshambuliaji huyo amewapiku wachezaji mwenzake wa Leicester,  Jamie Vardy na N'Golo Kante katika kinyang'anyiro cha tuzo hiyo sambamba na mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane, kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil na wa West Ham, Dimitri Payet.
    Vardy ameshika nafasi ya pili katika kura, wakati Kane amekuwa wa tatu. Mshambuliaji huyo wa Leicester pia alipewa tuzo maalum kwa kuvunja rekodi ya kufunga mabao katika mechi 11 mfululizo.

    Nyota wa Leicester City, Riyad Mahrez akiwa na tuzo yake ya Mchezaji Bora wa PFA wa Ligi Kuu ya England 2016 baada ya kukabidhiwa usiku wa kuamkia leo PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    REKODI YA MSIMU YA RYAD MAHREZ LIGI KUU

    Mechi alizocheza: 34
    Mabao aliyofunga: 17
    Pasi za mabao: 11 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAHREZ NDIYE MWANASOKA BORA WA MWAKA LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top