• HABARI MPYA

  Saturday, April 09, 2016

  WINGA WA NIGER ANAANZA YANGA NA AHLY LEO

  Issoufou Boubacar anaanza leo katika mchezo dhidi ya Al Ahly ya Misri leo

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluim amemuanzisha kiungo wa kimataifa wa Niger, Issoufou Boubacar katika mchezo dhidi ya Al Ahly ya Misri leo.
  Yanga inashuka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Saa 10:00 jioni ya leo kumenyana na Al Ahly katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya timu hizo kurudiana Aprili 19 mjini Cairo.
  Na Pluijm amefanya marekebusho madogo kutoka kikosi chake maarufu kilichokuwa kikicheza mechi za hivi karibuni.
  Kiungo Salume Telela amechukua nafasi ya Pato Ngonyani pale chini na winga Issoufou Boubacar amechukua nafasi ya Simon Msuva upande wa kushoto wa Uwanja.
  Safu ya ulinzi ya Yanga inaendelea kuwa vile vile ikiundwa na kipa Ally Mustafa ‘Barthez’, beki wa kulia Juma Abdul, kushoto Mwinyi Mngwali, katikati Vincent Bossou na Kevin Yondan. 
  Kikosi kamili cha Yanga leo ni; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Vincent Bossou, Kevin Yondan, Salum Telela, Deusi Kaseke, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Issoufou Boubacar.
  Benchi; Deo Munishi ‘Dida’, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Pato Ngonyani, Paul Nonga, Godfrey Mwashuya na Simon Msuva.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WINGA WA NIGER ANAANZA YANGA NA AHLY LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top