• HABARI MPYA

  Saturday, April 09, 2016

  MMAREKANI AWASILI DAR KUINOA TIMU YA TAIFA YA KIKAPU

  Na Renatha Msungu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mmarekani wa timu ya mpira wa Kikapu Matthew Mc Colister amewasili jijini juzi usiku kwa ajili ya kuanza rasmi kuinoa timu ya taifa ya mchezo huo inayojiandaa kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa.
  Matthew anatarajia kusaini mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili ya kuinoa timu hiyo ya taifa ambayo haijashiriki kwa muda mrefu mashindano makubwa ya kimataifa ukiacha ya Afrika Mashariki.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE jana, Mjumbe wa Kamati ya Ufundi wa Shirikisho la mpira wa kikapu nchini (TBF), Manase Zabron alisema, Kocha huyo ambaye ni raia wa Marekani,anatarajia kutembelea uwanja wa JK uliopo kidongo Chekundu, huku akianza rasmi kuangalia programu za wachezaji chipukizi, wakati akisubiri kusaini mkataba wake wa kuanza kuinoa timu ya taifa.


  Kocha wa mpira wa Kikapu, Matthew Mc Colister (kushoto) akiwa na 

  Manase alisema mara baada ya zoezi hilo kukamilika,MC Colister ataendelea na zoezi zima la kuanza kuinoa timu hiyo pamoja na vijana ambao anaamini wtakuwa wazuri hapo baadae.
  Naye Colister alisema amewasili jijini kwa lengo moja tu la
  kuhakikisha anapandisha viwango vya wachezaji ili waweze kuwa wa kimataifa. Alisema lengo lake ni kuona timu atakayoifundisha inasonga mbele
  kiuchezaji na kuweza kutoa ushindani mkali kwa timu ambazo watakutana nazo katika michuano ya mchezo huo ya Kimataifa. Alisema anaamini Tanzania kuna vipaji vingi vya wachezaji, ispokuwa wanakosa nafasi ya kuviendeleza.
  Alisema baada yeye kuwasili, anaamini timu hiyo itakuwa bora kama zilivyo za nchi nyingine.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MMAREKANI AWASILI DAR KUINOA TIMU YA TAIFA YA KIKAPU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top