• HABARI MPYA

  Friday, April 15, 2016

  ULIMWENGU AENDELEA KUNG’ARA TP MAZEMBE

  Na Mwandishi Wetu, KINSHASA
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu (pichani kushoto) ameendelea kuonyesha umuhimu wake katika klabu ya TP Mazembe ya DRC baada ya usiku wa Alhamisi kufunga bao katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Shark XI FC.
  Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo uliofanyika Uwanja wa Martys mjini Kinshasa, Ulimwengu maarufu kwa jina la Rambo mjini Lubumbashi, makao makuu ya Mazembe, alifunga bao hilo dakika ya 68 baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Rogger Asale dakika ya 57.
  Na Ulimwengu alifunga bao hilo akimalizia pasi ya Rainfrod Kalaba, wakati bao la kwanza la mabingwa hao wa Afrika lilifungwa na Luyindama dakika ya 65 kwa pasi ya Joseph Bolingi.
  Mazembe inarejea Lubumbashi kujiandaa na mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco Aprili 20.
  Mazembe inahitaji ushindi wa 3-0 ili kusonga mbele baada ya kufungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza mwishoni mwa wiki mjini Casablanca.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ULIMWENGU AENDELEA KUNG’ARA TP MAZEMBE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top