• HABARI MPYA

  Friday, April 15, 2016

  MRISHO NGASSA AFIWA NA MDOGO WAKE MWANZA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amefiwa na mdogo wake, aitwaye Rama mjini Mwanza.
  Baba wa Mrisho, Khalfan Ngassa ‘Babu’ ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo kwamba Rama amefariki jana jioni na anatarajiwa kuzikwa leo mchana, baada ya sala ya Ijumaa.
  Babu Ngassa, kiungo wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba ya Dar es Salaam, amesema kijana huyo amefariki dunia baada ya kuugua kwa siku mbili.
  Akizungumza kutoka Bethlehem, Afrika Kusini anakochezea klabu ya Free State Stars ya Ligi Kuu ya ABSA, Ngassa amesema kwamba amezipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo.
  Mrisho Ngassa amefiwa na mdogo wake aitwaye Rama mjini Mwanza

  Marehemu Rama enzi za uhai wake
  “Rama ni mtu ambaye amekuwa akisimamia vitu vyangu na mambo au shughuli zangu zote za Mwanza, ni mtu ambaye amekuwa akiawaangalia wazazi pale. Kwa kweli ni pigo sana,”amesema Ngassa ambaye kwa sasa ni majeruhi.
  Nyota huyo wa zamani wa Toto Africans ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba, Azam, Simba na Yanga za Dar es Salaam amesema asubuhi hii anakutana na uongozi wa Free State kupanga taratibu za kurejea nyumbani kwa ajili ya msiba.
  “Sijui kama nitawahi mazishi, lakini sitaki nichelewe sana,”amesema Mrisho.

  BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE inampa pole Mrisho, familia yake na wote walioguswa na msiba huo. Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Rama. Amin.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MRISHO NGASSA AFIWA NA MDOGO WAKE MWANZA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top