• HABARI MPYA

  Wednesday, April 20, 2016

  SAMATTA ATOKA KAPA GENK IKISHINDA 4-2

  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta (pichani kushoto) leo amecheza kwa dakika 74, timu yake, KRC Genk ikishinda 4-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji Uwanja wa Cristal Arena mjin Genk.
  Samatta alitolewa dakika ya 74 kumpisha mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis wakati huo tayari Genk inaongoza 4-0.
  Mabao ya Genk yamefungwa na beki Mnigeria, Onyinye Wilfred Ndidi dakika ya 15, kiungo Mspanyola Alejandro Pozuelo dakika ya 42, beki Mbelgiji, Thomas Meunier aliyejifunga dakika ya 45 na ushei na beki Mfinland, Jere Uronen dakika ya 73.
  Mabao ya Club Brugge limefungwa na kiungo Mholanzi, Ruud Vormer dakika ya 80 na Thomas Meunier dakika ya 84.
  Huo unakuwa mchezo wa 10 kwa Samatta tangu ajiunge na Genk Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DRC, akiwa amefunga mabao nne. 
  Samatta alifunga bao moja katika ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem mwishoni mwa wiki baada ya awali kufunga katika ushindi wa 4-0 na 4-1 dhidi ya KV Oostende na 3-2 dhidi ya Club Brugge.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ATOKA KAPA GENK IKISHINDA 4-2 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top