• HABARI MPYA

  Friday, April 08, 2016

  SAMATTA AFUNGA TENA GENK IKIUA 4-0 UBELGIJI

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ametokea benchi na kuifungia timu yake, KRC Genk katika ushindi wa 4-0 dhidi ya KV Oostende kwenye mchezo wa Loigi Ku ya Ubelgiji usiku huu.
  Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Cristal Arena, mjini Genk, Nahodha wa Tanzania, Samatta alifunga bao hilo dakika ya 77, ikiwa ni dakika moja tu baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis.
  Mbwana Samatta amefunga bao lake la tatu leo KRC Genk ikishinda 4-0

  Mabao mengine ya Genk yamefungwa na Pozuelo dakika ya 12, T. Buffel dakika ya 21 na N. Kebano dakika ya 85.
  Hilo linakuwa bao la tatu kwa Samatta katika mechi nane alizocheza tangu ajiunge na Genk Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DRC.  
  Kabla ya kufunga katika ushindi wa 4-1 dhidi ya KV Oostende, Samatta pia alifunga katika ushindi wa 3-2 baada ya kuingia dakika 15 za mwisho dhidi ya Club Brugge.
  Mechi nyingine alizocheza Samatta tangu atue Genk, zote akitokea benchi dakika za mwishoni ni dhidi ya Standard Liege (Genk) wakifungwa 2-1, dhidi ya Lokeren wakitoa sare ya 0-0, dhidi ya Waasland-Beveren wakishinda 6-1 na dhidi ya Mouscron-Peruwelz wakishinda 1-0 pia ugenini na dhidi ya Anderlecht wakifungwa 1-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AFUNGA TENA GENK IKIUA 4-0 UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top