• HABARI MPYA

  Wednesday, April 13, 2016

  RONALDO MPE HESHIMA YAKE, AWAPIGA TATU WAJERUMANI, REAL YATINGA NUSU FAINALI

  MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro ameipeleka Real Madrid Nusu Fainali ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya sita mfululizo baada ya kufunga mabao matatu yake, ikishinda 3-0 usiku huu Uwanja wa Santiago Bernabeu mjini Madrid dhidi ya Wolfsburg ya Ujerumani.
  Real inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya wiki iliyopita kufungwa 2-0 Ujerumani.
  Ronaldo alifunga mabao hayo katika dakika za 15, 17 na 77 na kufikisha mabao 46 msimu huu kwenye mashindano yote.
  Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kukamilisha hat-trick dhidi ya Wolfsburg PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Mchezi mwingine wa Robo Fainali usiku huu, bao pekee la Kevin de Bruyne dakika ya 14 Uwanja wa Etihad limetosha kuipeleka Manchester Nusu Fainali kwa mara ya kwanza katika historia yao kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya PSG.
  City inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya wiki iliyopita kulazimisha sare ya 2-2 mjini Paris.
  City ingepeta ushindi mzuri zaidi kama si mshambuliaji Sergio Aguero kupaisha mkwaju wa penalti baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na kipa wa PSG, Kevin Trapp
  Ajabu kipa Mjerumani, Trapp alionyeshwa tu kadi ya njano kwa rafu hiyo licha ya kabisa kumzuia mshambuliaji huyo wa City akiwa katika nafasi ya kufunga.
  Kocha Manuel Pellegrini sasa anaweza kukutana na mrithi wake mwishoni mwa msimu, Pep Guardiola iwapo Bayern Munich itaingia Nusu Fainali.
  Kevin de Bruyne (kulia) akishangilia baada ya kuifungia Manchester City bao pekee la ushindi PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Robo Fainali za mwisho zinachezwa usiku wa Jumatano Atletico Madrid wakiikaribisha Barcelona, zote za Hispania Uwanja wa Vicente Calderon na Benfica ya Ureno wakiwa wenyeji wa Bayern Munich Uwanja wa Luz. Mechi za kwanza wiki iliyopita, Bayern ilishinda 1-0 na Barcelona ilishinda 2-1.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO MPE HESHIMA YAKE, AWAPIGA TATU WAJERUMANI, REAL YATINGA NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top