• HABARI MPYA

  Tuesday, April 12, 2016

  NI YANGA NA COASTAL, AZAM NA MWADUI NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

  ORODHA YA MABINGWA KOMBE LA SHIRIKISHO
  1967    Yanga SC 
  1974    Yanga SC
  1985    Maji Maji
  1995    Simba SC
  1996    Sigara
  1997    Tanzania Stars
  1998    Tanzania Stars
  1999    Yanga SC
  2000    Mtibwa Sugar
  2001    Yanga SC 
  2002    JKT Ruvu 
  Ofisa Habari wa TFF, akimshuhudia mchezaji wa zamani wa Twiga Stars, Esther Chabruma 'Lunyamila' akichagua timu za kumenyana katika Nusu Fainali ya Kombe la Azam Sports Federation Cup mwaka huu

  Na Saada Mohammed, DAR ES SALAAM
  YANGA SC itamenyana na Coastal Union katika Nusu Fainali ya michuano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federations Cup 2016.
  Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga Aprili 24, mwaka huu, siku ambayo Azam FC itamenyana na Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga Aprili 24, mwaka huu pia. 
  Hiyo inafuatia droo iliyopangwa leo studio za Azam TV, wadhamini wa michuano hiyo, Tabata, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa.
  Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, Esther Chabruma ndiye aliyechagua timu za kumenyana katika Nusu Fainali katika droo hiyo, akisimamiwa na Ofisa Habari wa TFF, Baraka Kizuguto.
  Coastal Union iliingia Nusu Fainali baada ya kuitoa Simba SC kwa kuifunga mabao 2-1, wakati Azam FC iliitoa Prisons kwa kuifunga 3-1, Mwadui FC iliitoa Geita Gold kwa kufunga 3-0 na Yanga SC iliwafunga Ndanda FC 2-1.
  Bingwa wa Kombe la ASFC, michuano iliyoanza na timu 64 Novemba mwaka jana, ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
  Katika hatua ya awali, kila timu ilipatiwa fedha za usafiri Sh Milioni 3, na vifaa vya mashindano kutoka kwa wadhamini, Azam TV ikiwa ni sehemu ya udhamini wa Bilioni 3.3.
  Bingwa wa Kombe la ASFC atajinyakuliwa kitita cha Sh. Milioni 50,
  Fainali inatarajiwa kuchezwa wiki moja baada ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kumalizika.
  Mara ya mwisho michuano hiyo ilifanyika mwaka 2002 na JKT Ruvu ikaifunga Baker Rangers ya Magomeni katika fainali, wakati ikijulikana kama Kombe la FAT (Chama cha Soka Tanzania).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI YANGA NA COASTAL, AZAM NA MWADUI NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top