• HABARI MPYA

  Monday, April 04, 2016

  MFARANSA ALIYEIPIGA TAIFA STARS 7-0 ABWAGA MANYAGA ALGERIA

  KOCHA aliyeiongoza Algeria kuitoa Tanzania katika mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia mwishoni mwa mwaka jana, Christian Gourcuff ameacha kazi kazi jana.
  Algeria ilitoa sare ya 2-2 na Taifa Stars Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Novemba 14, kabla ya kwenda kushinda 7-0 Novemba 17 mwaka jana Uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida.
  Na kocha aliyeifanyia 'unyama' huo Tanzania amewakimbia Algeria baada ya kufanya kazi kwa zaidi ya miaka miwili akiipa mafanikio makubwa nchi hiyo kiasi cha kuwa namba moja kwa ubora wa soka Afrika.

  Christian Gourcuff aliiongoza Algeria kuifunga 7-0 Tanzania katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia Novemba mwaka jana 

  Shirikisho la Soka Algeria limetangaza kuondoka kwa mwalimu huyo kupitia tovuti yao, wakisema wamevunja Mkataba wake kwa maombi yake.
  Mfaransa huyo aliwaambia mabosi wake baada ya kurejea kutoka Ethiopia kwenye mechi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika kwamba anatarajia kuondoka Alhamisi.
  Baada ya kushinda mechi tatu na sare moja, Algeria imejiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu fainali zijazo za AFCON 2017, ikihitaji ushindi mmoja zaidi katika mechi zake zilizobaki dhidi ya Shelisheli ugenini Juni 3 na Lesotho nyumbani Septemba 2 kujihakikishia kufuzu.
  Mwanasoka huyo wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, alianza kazi mwaka 2014.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MFARANSA ALIYEIPIGA TAIFA STARS 7-0 ABWAGA MANYAGA ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top