• HABARI MPYA

    Tuesday, April 05, 2016

    BOSI WA ZAMANI MAN CITY AWA MWENYEKITI MTENDAJI AFRICAN LYON

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KLABU ya African Lyon ya Dar es Salaam imepata Mwenyekiti mpya Mtendaji, ambaye mfanyabiashara mwenye wa Asia, Dk Sulaiman Al-Fahim (pichani kushoto).
    Mmiliki wa African Lyon iliyopanda tena Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Rahim Kangezi amesema kwamba Dk. Al- Fahim amekubali ombi la kuwa kiongozi mkuu wa klabu hiyo ya zamani ya mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubelgiji, Samatta baada ya kuombwa kwa miaka minne sasa.
    Kangezi amesema waliamua kumuomba Al Fahim kuwa kiongozi mkuu wa klabu yao si kwa sababu mfanyabiashara mkubwa na bilionea nchi za Uarabuni na duniani kwa ujumla, bali pia kutokana na uzoefu wake katika michezo, hususan soka. 

    Dk Sulaiman Al-Fahim (kulia) akiwa na jezi ya kampuni ya Abu Dhabi United, wamiliki wa Manchester City

    Amesema Al- Fahim ni Rais wa kampuni ya Arab Union for Real Estate Development ya Dubai baasa ya awali kuwa Msemaji wa kampuni Abu Dhabi United Group (ADUG), wamiliki Manchester City ya England walioinunua Septemba, 2008.
    Kangezi amesema Al- Fahim aliyejaribu bila mafanikio kununua Portsmouth iliyowahi kushiriki Ligi Kuu England, ataanza kazi rasmi African Lyon Aprili 16 kwa kutangaza timu atakayofanya nayo kazi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BOSI WA ZAMANI MAN CITY AWA MWENYEKITI MTENDAJI AFRICAN LYON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top