• HABARI MPYA

  Monday, April 04, 2016

  BLACKWELL AZINDUKA SIKU TISA BAADA YA KIPIGO CHA 'NUSU AFE' ULINGONI

  BONDIA Nick Blackwell hatimaye amezinduka baada ya kuwa mahututi na sasa ameanza kuzungumza na familia yake na marafiki akiwa kitandani katika hospitali aliyolazwa.
  Bwana mdogo huyo wa umri wa miaka 25 amekuwa mahututi tangu apate kipigo 'cha kufa mtu' kutoka kwa Chris Eubank Jnr kiasi cha damu kuvujia kwenye ubongo katika pambano la ubingwa wa dunia uzito wa Middle siku tisa zilizopita.
  Bondia huyo pia anapumua vizuri kuashiria anaendelea kupata nafuu.
  Taarifa ya promota wake, kampuni ya Hennessy Sports imesema: "Mwishoni mwa wiki, Nick amezinduka kwenye hali mbaya, akianza kuzungumza na wapendwa wake, kufika Jumapili, alianza kuzungumza.

  Nick Blackwell hatimaye amezinduka na kuanza kuzungumza na familia yake na marafiki 

  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BLACKWELL AZINDUKA SIKU TISA BAADA YA KIPIGO CHA 'NUSU AFE' ULINGONI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top