• HABARI MPYA

    Wednesday, April 06, 2016

    MAZOEZI YANGA MIPANGO MITUPU PEMBA, TENA ILE YA LAZIMA ‘MWARABU AFE’ TAIFA

    Viungo wa Yanga, Mzimbabwe Thabani Kamusoko (kushoto) na Mkongo Mbuyu Twite wakipeana maji baada ya mazoezi ya leo asubuhi Uwanja wa Gombani

    Na Abdallah Salim, PEMBA
    YANGA SC inaendelea vizuri na mazoezi yake kujiandaa na mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa ya Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mabingwa wa Tanzania Bara wameweka kambi katika hoteli ya kitalii ya Misali Sun Set Beach, Chake Chake, Pemba tangu Jumatatu kujiandaa na mchezo unaosubiriwa kwa hamu. 
    Yanga imekuwa na vipindi viwili vya mazoezi katika siku mbili za mwanzo, kwanza ufukwe wa hoteli ya Misali Sun Set Beach asubuhi na jioni Uwanja wa Gombani.
    Lakini kaunzia leo wamefanya mazoezi ya asubuhi Gombani ambako wanatarajiwa kurudi na jioni pia.

    Mshambuliaji Malimi Busungu baada ya mazoezi ya leo asubuhi Gombani

    Kutoka kulia Kevin Yondan, Deus Kaseke na Oscar Joshua baada ya mazoezi ya leo asubuhi

    Na katika mazoezi hayo, Kocha Mkuu, Mhoalnzi, Hans van der Pluijm ameonekana zaidi akiwaelekeza wachezaji mbinu za kuzuia na kushambulia.
    Pluijm pia amekuwa akifanyia kazi makosa ambayo yamekuwa yakijitokeaa katika mechi zilizopita katika safu ya ulinzi na kiungo, wakati pia ameonekana kuwa mkali kwa washambuliaji wanaopoteza nafasi. 
    Kikosi cha Yanga ambacho kipo kambini Pemba ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benedicto Tinocco.
    Mabeki ni Juma Abdul, Oscar Joshua, Mwinyi Hajji Mngwali, Pato Ngonyani, Kevin Yondan, Vincent Bossou (Togo) na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
    Viungo ni Salum Telela, Mbuyu Twite (DRC), Said Juma ‘Makapu’, Thabani Kamusoko (Zimbabwe), Haruna Niyonzima (Rwanda), Simon Msuva, Deus Kaseke, Godfrey Mwashiuya na Issoufou Boubacar (Niger).
    Washambuliaji ni Paul Nonga, Matheo Anthony, Malimi Busungu, Amissi Tambwe (Burundi) na Donald Ngoma (Zimbabwe). 
    Benchi la Ufundi ni Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm (Uholanzi), Kocha Msaidizi, Juma Mwambusi, Kocha wa makipa, Juma Pondamali
    Daktari, Edward Bavu, Mchua Misuli, Jacob Onyango, Mtunza Vifaa, Mohammed Mpogolo na 
    Meneja, Hafidh Saleh. 
    Wapinzani wao, Al Ahly wamewasili alfajiri ya leo Dar es Salaam na jioni wanatarajiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana.
    Timu hiyo ya kocha Mholanzi, Maarten Cornelis Jol maarufu kama Martin Jol, imewasili na wachezaji 21 ambao ni makipa; Ahmed Abdul Monem, Mosaad Awad, Sherif Ekramy.
    Mabeki; Ahmed Fathy, Bassem Ali, Mohamed Hany, Rami Rabia, Saad Samir, Ahmed Hagazy na Sabri Rahil.
    Viungo; Amir El-Sulaya, Ahmed El El- Sheikh, Walid Soliman, Abdalla El Said, Hossam Ghaly, Hossam Ashour, Ramadan Sobhi na Momen Zakaria.
    Washambuliaji; Malick Evouna, Emad Moteab na Amr Gamal.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAZOEZI YANGA MIPANGO MITUPU PEMBA, TENA ILE YA LAZIMA ‘MWARABU AFE’ TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top