• HABARI MPYA

  Wednesday, April 06, 2016

  KOCHA WA YANGA ATUPIWA VIRAGO TOGO, LEROY ACHUKUA NAFASI

  KOCHA wa zamani wa Yanga, Mbelgiji Tom ameondolewa timu ya taifa ya Togo na nafasi yake inachukuliwa na Mfaransa, Claude LeRoy.
  Kwa mujibu wa gazeti la michezo Ufaransa, L’Equipe kocha LeRoy amesaini Mkataba wa miaka mitatu hadi mwaka 2019 na atafanya kazi na Msaidizi wake wa muda mrefu, Sebastien Minier.
  Togo kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika Kundi A kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Gabon, ikizidiwa pointi mbili na vinara, Liberia, ambao watakutana nao katika mchezo ujao ugenini Juni. 

  Timu hiyo iliambulia pointi moja katika mechi mbili za nyumbani na ugenini na Tunisia mwezi uliopita na Novemba ilitolewa katika mchujo wa kuwania nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia Urusi kwa kufungwa jumla ya mabao 4-0 na Uganda.. 
  Le Roy, mwenye umri wa miaka 68, anatarajiwa kumshawishi mshambuliaji Emmanuel Adebayor kurejea timu ya taifa baada ya nyota huyo wa Crystal Palace ya England kukosa mchezo wa ugenini na Tunisia kabla ya kucheza wa marudiano nyumbani.
  Le Roy amekuwa akifanya kazi barani Afrika kwa miaka karibu 30 na anashikilia rekodi ya kufundisha timu timu nane katika Fainali za Mataifa ya Afrika zikiwemo Senegal, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC naCameroon aliyoipa ubingwa mwaka 1988.
  Ana rekodi ya mechi 35 kwenye fainali hizo na ni mara moja tu alikuwa ana timu ikashindwa kufuzu fainali za AFCON.
  Aliifikisha Kongo Robo Fainali katika fainali za Equatorial Guinea Januari, kabla ya kujiuzulu Novemba mwaka jana licha ya kuiweaesha nchi hiyo kusonga mbele kwenye mechi za kufuzu Kombe la Dunia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA WA YANGA ATUPIWA VIRAGO TOGO, LEROY ACHUKUA NAFASI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top