• HABARI MPYA

    Wednesday, April 06, 2016

    TFF YAAHIDI KUWASHUGHULIKIA WATU WA MIPANGO MICHAFU

    Rais wa TFF, Jamal Malinzi
    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeahidi kuwachukukliwa hatua maofisa wake waliohusika katika mpango mchafu wa kuisaidia timu moja ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
    Sauti za kurekodiwa za Maofisa wa TFF wakiwa kwenye kikao cha pamoja na viongozi wa timu moja ya daraja la kwanza na zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao tangu jana. 
    Na Taarifa ya TFF leo imesema kwamba pamoja na kwamba taarifa hizo zilizosambazwa hazihusiani na kesi ya kupanga matokeo iliyoamuliwa siku ya tarehe 03/04/2016, TFF inachunguza kubaini uhalisia (authenticity) wa taarifa hizo na itachukua hatua kali sana kwa watumishi wa shirikisho na viongozi wa timu husika watakaobainika kushiriki vitendo vilivyo kinyume na maadili ya mpira wa miguu.
    TFF imekwishaweka bayana nia ya kupambana na yeyote atakayehusika katika upangaji matokeo na uhalifu mwingine unaoharibu ustaarabu wa mpira kwa njia yoyote ile.
    TFF pia linatoa onyo kwa baadhi ya viongozi, watumishi wa TFF na wadau wa mpira wa miguu kwa ujumla wanaotumia majina ya viongozi wa juu wa TFF katika kufanikisha mipango yao kwa manufaa binafsi.
    TFF imewaomba wapenda mpira wa miguu kuwa watulivu na waangalifu wakati  suala hili linashughulikiwa.
    Aidha, kuhusu hukumu ya Kamati ya Nidhamu ya TFF ni muhimu ikaeleweka wazi kwamba zipo taratibu za kukata rufaa kwa mujibu wa kanuni ili upande usioridhika na maamuzi yanayotolewa uweze kuhoji maamuzi husika.
    Ni vema tukaacha kamati huru zifanye kazi zake kwa mujibu wa taratibu. Kutoa hukumu  mtaani au kwenye vyombo vya habari kunaweza kuwanyima haki wanaostahili na kutengeneza kichaka cha kujificha watenda maovu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAAHIDI KUWASHUGHULIKIA WATU WA MIPANGO MICHAFU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top