• HABARI MPYA

  Monday, April 11, 2016

  MAYANJA AMPA ‘KIGODA’ KIIZA SIMBA NA COASTAL

  Na Saada Mohammed, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mganda, Jackson Mayanja amemuanzishia benchi kinara wa mabao wa timu hiyo, Hamisi Friday Kiiza katika mchezo wa leo dhidi ya Coastal Union.
  Simba wanamenyana na Coastal jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup.
  Na Mayanja amewaanzisha pamoja washambuliaji Ibrahim Hajib na Danny Lyanga, wakati beki Hassan Kessy amempanga wingi ya kulia.

  Hamisi Friday Kiiza anaanzia benchi dhidi ya Coastal Union leo

  Kikosi kamili cha Simba ni; Vincent Angban, Emery Nimubona, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Novaty  Lufungo, Justice Majabvi, Hassan Kessy, Jonas Mkude, Danny Lyanga, Ibrahim Hajibu na Said Ndemla.
  Benchi; Peter Manyika, Awadh Juma, Mussa Mgosi, Juuko Murshid, Peter Mwalyanzi, Hamisi Kiiza na Paul Kiongera.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYANJA AMPA ‘KIGODA’ KIIZA SIMBA NA COASTAL Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top