• HABARI MPYA

  Monday, April 11, 2016

  MICHUANO YA COSAFA U20 YAFUFUKA

  KAMPUNI ya usambazaji wa saruji Afrika Kusini, PPC imejitolea kudhamini michuano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kusini mwa Afrika, COSAFA ambayo imeshindwa kufanyika kwa miaka miwili iliyopoita.
  Michuano hiyo inarudi mwaka huu na itafanyika jimbo la Kaskazini Magharibi mwa Afrika Kusini mwezi Desemba na PPC wamepewa fursa ya kurefusha udhamini wao kwa miaka mitatu.
  Mkuu wa Idara ya Masoko ya PPC, Rob Rein amesema kwamba udhamini huo ni sehemu ya kusherehekea miaka yao 124 ya mafanikio katika kutoa huduma ya saruji na pia wamedhamiria kuinua vipaji.
  Rais wa COSAFA, Suketu Patel ameishukuru PPC kwa udhamini huo unaosaidia kuzalisha nyota wa kesho wa soka
  Michuano hiyo ambayo imekuwa ikifanyika kwa miaka 33 sasa imeibua nyota kibao kama Itumeleng Khune, Lerato Chabangu, Daine Klate na Lebohang Mokoena wa Afrika Kusini, Clifford Mulenga na Isaac Chansa wa Zambia, Tinashe Nengomasha na Onismor Bhasera wa Zimbabwe sambamba na Jimmy Zakazaka wa Malawi.
  Michuano iliyopita ilifanyika nchini Lesotho mwaka 2013, ambako Afrika Kusini iliwafunga wageni waalikwa Kenya 2-0 katika fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MICHUANO YA COSAFA U20 YAFUFUKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top