• HABARI MPYA

  Monday, April 11, 2016

  HANS POPPE KUONGOZA KAMATI YA UJENZI BUNJU COMPLEX

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  RAIS wa klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Evans Elieza Aveva amemteua Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Zacharia Hans Poppe (pichani kulia) kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Ujenzi wa Uwanja Bunju Complex.
  Katika taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Simba, kazi kubwa ya Kamati hiyo itakuwa kuratibu shughuli zote za ujenzi wa Uwanja ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha za ujenzi unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.
  Mbali na Hans Poppe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Aveva amemteua Salim Muhene, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji kuwa Makamu wa Mwenyekiti.
  Katibu ni Issa Batenga wakati Wajumbe wa Kamati hiyo ni Ally Suru, ambaye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Adam Mgoyi ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini, Crescentius Magori, Imani Kajula na Jerry Yambi.
  Kamati hiyo inatarajiwa kukutana Waandishi wa Habari kuelezea mikakati yao juu ya majukumu waliyopewa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HANS POPPE KUONGOZA KAMATI YA UJENZI BUNJU COMPLEX Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top