• HABARI MPYA

  Monday, April 11, 2016

  FARID HATAKUWEPO MECHI YA MARUDIANO NA ESPERANCE, ANAKWENDA ULAYA

  Na Saada Mohammed, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Azam FC itamkosa kiungo Farid Mussa Malik (pichani kushoto) katika wa mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance mjini Tunis wiki ijayo.
  Baada ya kufunga bao la kusawazisha katika ushindi wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam – Farid sasa anajiandaa kwa safari ya majaribio Ulaya.
  Bado wakala wa Farid hajaweka wazi basi anampeleka wapi kijana huyo, lakini inaelezwa atampeleka au Ubelgiji, Scotland au Hispania ambako kote kuna timu za kumjaribu.
  Esperanace jana ndiyo waliotangulia kupata bao lao dakika ya 33 kupitia kwa Haithem Jouini, kabla ya Farid kuisawazishia Azam dakika ya 68 na Ramadhani Singano ‘Messi’ kufunga la ushindi dakika ya 70. 
  Azam FC inayomilikiwa na Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake, sasa inatakiwa kwenda kulazimisha sare yoyote ugenini katika mchezo wa marudiano wiki ijayo ili kwenda hatua ya mwisho ya kuwania kucheza hatua ya makundi
  Wakati huo huo: 
  Kocha Msaidizi wa Azam, Denis Kitambi amesema kutokuwepo kwa beki wao Shomary Kapombe kuliwafanya jana wabadili mfumo na kucheza 4-3-3 badala ya 5-2-3.
  Kapombe ni mgonjwa na kwa sasa yuko Afrika Kusini ambako anapatiwa matibabu na atakosekana pia kwenye mchezo wa marudiano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FARID HATAKUWEPO MECHI YA MARUDIANO NA ESPERANCE, ANAKWENDA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top