• HABARI MPYA

    Tuesday, April 05, 2016

    CONTE ASAINI MIAKA MITATU CHELSEA KUMRITHI MOURINHO

    Chelsea imemtangza Antonio Conte kuwa kocha mpya baada ya kumfukuza Jose Mourinho  PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    WASIFU WA ANTONIO CONTE   

    MATAJI ALIYOSHINDA AKIICHEZEA JUVENTUS
    Serie A: 1995, 1997, 1998. 2002, 2003
    UEFA Cup: 1993
    Ligi ya Mabingwa: 1996 
    MATAJI ALIYOSHNDA AKIWA KOCHA 
    Juventus: Serie A (2012, 2013, 2014)
    Bari: Serie B (2009) 
    HISTORIA YAKE YA UKOCHA 
    Arezzo: 2006 - 2007
    Bari: 2007 - 2009
    Atalanta: 2009- 2010
    Siena: 2010- 2011
    Juventus: 2011 - 2014
    Italia: 2014-16
    HATIMAYE Chelsea imemtangaza rasmi Mtaliano Antonio Conte kuwa kocha wake mpya atakayerithi mikoba ya Jose Mourinho.
    Chelsea imetangza Conte Jumatatu kwamba amesaini Mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Pauni Milioni 20.
    Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 46 alipata umaarufu alipokuwa anaifundisha Juventus kabla ya kuwa kocha wa timu ya taifa ya Italia.
    Conte sasa anatarajiwa kuhamishia mafanikio yake Stamford Bridge baada ya Chesela kupitia msimu mbaya zaidi tangu inunuliwe nabilionea Mrusi, Roman Abramovich.
    Dau lake linahusisha mshahara wa Pauni Milioni 6.5 na posho ya Pauni Milioni 5 akishinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. 
    Lakini jukumu lake la kwanza na kuipeleka klabu katika michuano ya Ulaya Europe. Kwa sasa Chelse ipo chini ya kocha wa muda, Guus Hiddink aliyepewa timu amalizie msimu baada ya kufukuzwa Mourinho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CONTE ASAINI MIAKA MITATU CHELSEA KUMRITHI MOURINHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top