• HABARI MPYA

    Tuesday, April 05, 2016

    BARCA, BAYERN ZAPATA USHINDI MWEMBAMBA NYUMBANI LIGI YA MABINGWA

    MABINGWA wa zamani wa Ulaya, Barcelona ya Hispania na Bayern Munich ya Ujerumani, zote zimepata ushindi mwembamba katika mechi zao za kwanza za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa nyumbani.
    Barcelona imewafunga washiriki wenzao wa La Liga ya Hispania, Atletico Madrid mabao 2-1 Uwanja wa Camp Nou, wakati Bayern Munich imeshinda 1-0 dhidi ya Benfica ya Ureno Uwanja wa Allianz Arena.
    mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na Chelsea za England, Fernando Torres alianza kuifungia  Atletico Madrid dakika ya 25, kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu dakika 10 baadaye kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano..
    Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez (kulia) akishangilia baada ya kuifungia timu yake usiku huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA

    Luis Suarez akaisawazishia Barca dakika ya 63 na kuifungia bao la ushindi dakika ya 74.
    Matokeo hayo, yanamaanisha Barca bado haipo salama, kwani inaweza kutolewa iwapo itafungwa 1-0 katika mchezo wa marudiano mjini Madrid.
    Bao pekee la Arturo Vidal mapema tu dakika ya pili limeipa ushindi wa 1-0 Bayern Munich dhidi ya Benfica. Bayern sasa wana kazi ya ziada ya kwenda kuulinda ushindi wao katika mchezo wa marudiano ugenini.
    Robo Fainali za pili zitachezwa kesho VfL Wolfsburg na Real Madrid Uwanja wa Volkswagen Arena na Paris Saint-Germain na Manchester City Uwanja wa Parc des Princes..
    Arturo Vidal akikimbia kushangilia baada ya kuifungia baon pekee Bayern Munich PICHA ZAIDI GONGA HAPA
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCA, BAYERN ZAPATA USHINDI MWEMBAMBA NYUMBANI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top