• HABARI MPYA

  Tuesday, April 05, 2016

  MKURUGENZI WA MASHINDANO ANG'ATUKA TFF

  KAIMU Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Martin Chacha (pichani kulia) amejiuzulu nafasi yake katika utumishi wa TFF kuanzia leo Aprili 5, 2016.
  Katika barua yake aliyomwandikia Katibu Mkuu wa TFF, Chacha amesema kwamba anaondoka baada ya kupata majukumu mapya ya kikazi ambayo pamoja na majukumu ya kifamilia, yatamfanya akose muda wa kutumika vema katika nafasi yake katika Shirikisho.
  Chacha alijiunga na TFF Julai 2014 akiwa Ofisa wa Mashindano na baadaye kuteuliwa kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Mashindano, kufuatia aliyekuwa anashikiria nafasi hiyo Boniface Wambura kuteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKURUGENZI WA MASHINDANO ANG'ATUKA TFF Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top