• HABARI MPYA

  Tuesday, April 12, 2016

  ALIYEWAZURU SIMBA JANA AOMBA TENA KAZI YANGA

  Youssouf Sabo anataka kurudi Yanga
  Na Saada Mohammed, DAR ES SALAAM
  MFUNGAJI wa mabao yote ya Coastal Union ikiilza Simba SC 2-1 jana na kuitupa nje ya michuano ya michuano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup leo ameomba tena kusajiliwa Yanga.
  Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 na klabu ya Cotton Sport ya Gorua, Youssouf Soba alikuwa Yanga mwishoni mwa mwaka jana kwa majaribio, lakini hakusajiliwa.
  “Nilikwenda Yanga kuomba kusajiliwa mwaka jana, nikafanya majaribio, lakini kocha akasema mimi ni mchezaji mzuri ila nafasi za wachezaji wa kigeni zimeisha,”amesema Youssouf Soba akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE jana.
  Soba aliyasema hayo mara tu baada ya mechi hiyo ya Robo Fainali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na akasema hata kama Azam wanamtaka, yuko tayari kuzungumza nao. 
  Sabo alifunga bao la kwanza dakika ya 19 kwa shuti la mpira wa adhabu umbali wa mita zaidi ya 20 na kutinga nyavuni moja kwa moja likimpita kipa Muivory Coast, Vincent Angban, kabla ya Mganda Hamisi Kiiza kutokea benchi kipindi cha pili na kuisawazishia Simba dakika ya 47.
  Hata hivyo, Sabo tena akaifungia Coastal bao la ushindi kwa penalti dakika ya 85, kufuatia beki Novaty Lufunga kumuangusha kwenye boksi mshambuliaji Ally Ahmed ‘Shiboli’.
  Kwa ushindi huo, Coastal imeungana na  Azam FC, Mwadui FC, na Yanga SC kukata tiketi ya kucheza Nusu Fainali.
  Droo ya Nusu Fainali inatarajiwa kufanyika leo Saa 3:00 usiku moja kwa moja kupitia chaneli ya Azam Two ya Azam TV.
  Robo Fainali za awali, Azam FC iliitoa Prisons kwa kuifunga 3-1, Mwadui FC iliitoa Geita Gold kwa kufunga 3-0 na Yanga SC iliwafunga Ndanda FC 2-1.
  Ikumbukwe bingwa wa Kombe la ASFC ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ALIYEWAZURU SIMBA JANA AOMBA TENA KAZI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top