• HABARI MPYA

    Tuesday, April 12, 2016

    SIMBA NA COASTAL KATIKA PICHA JANA

    Beki wa Coastal Union, Adeyoum Saleh Ahmed (kushoto) akikimbilia mpira dhidi ya mshambuliaji wa Simba, Hamisi Friday Kiiza katika mchezo wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Coastal ilishinda 2-1 na kwenda Nusu Fainali

    Beki wa Coastal Union, Mbwana Hamisi 'KIbacha' akijaribu bila mafanikio kuutelezea mpira miguuni mwa mshambuliaji wa Simba, Paul Kiongera

    Kiungo wa Simba, Jonas Mkude (kulia) akiwania mpira dhidi ya mshambuliaji wa Coastal, Youssouf Soba

    Hamisi Kiiza wa Simba (kulia) akitafuta maarifa ya kumpita Mbwana Hamisi 'Kibacha' wa Coastal

    Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Hajib (kulia) akitafuta maarifa ya kuwapita wachezaji wa Coastal Union

    Beki wa Coastal Hamad Juma (kushoto) akiuzuia mpira uliopigwa na mshambuliaji wa Simba, Danny Lyanga
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA COASTAL KATIKA PICHA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top