• HABARI MPYA

    Friday, March 18, 2016

    JKU KUIGEUZIA KIBAO VILLA LEO?

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Afrika, timu za Azam FC, JKU na Yanga SC katika michezo yao watakayocheza wikiendi hii.
    Katika salamu hizo, TFF imezitakia kila la kheri timu hizo kuhakikisha zinafanya vizuri katika michezo yao ili ziweze kusonga mbele katika hatua inayofuata, na kuwapa furaha washabiki wa mpira wa miguu pamoja na watanzania wote.
    JKU ya visiwani Zanzibara leo Ijumaa watakua kibaruani kuchuana na SC Villa ya Uganda, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Amani mjini Zanzibar baada ya kufungwa 4-0 katika mchezo wa kwanza Kampala.
    JKU inatakia kushinda 5-0 dhidi ya SC Villa ya Uganda ili kusonga mbele

    Kesho Jumamosi, Yanga SC watakua wenyeji wa APR ya kutoka nchini Rwanda katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa (CAF CL) kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, mchezo utakaochezeshwa na mwamuzi Bernard Camille, akisaidiwa na Eldrick Adelai, Gerard Pool na Allister Bara kutoka nchini Shelisheli.
    Jumapili Azam FC watakua wakicheza dhidi ya Bidvest FC kutoka nchini Afrika Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (CAF CC) kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, mwamuzi wa mchezo huo ni Gait Oting akisaidiwa na Abdallah Gassim, Casim Dehiya, mwamuzi wa akiba Ariel James wote kutoka Sudan Kusini
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JKU KUIGEUZIA KIBAO VILLA LEO? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top