• HABARI MPYA

  Tuesday, March 01, 2016

  WAHABESHI KUCHEZESHA MECHI YA TWIGA NA ZIMBABWE KUFUZU FAINALI ZA AFRIKA

  MAREFA kutoka Ethiopia ndiyo watakaochezesha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake kati ya wenyeji, Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Zimbambwe Ijumaa wiki hii Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Hao ni Lidya Tafesse atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na Yehuzewdubizua Yehuw na Tsige Sisay watakaoshika vibendera, wakati refa wa mezani atakuwa Woinshetkassaye Abera na Kamisaa Geneviev Kanjika kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Kila la heri Twiga Stars kuelekea mchezo na ZImbabwe kufuzu Fainali za Afrika

  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto amesema kwamba maofia hao wote wanatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Alhamisi mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya, (KQ).
  Kizuguto pia ametaja viingilio vya mchezo huo, Sh, 2,000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 3,000 kwa jukwaa kuu.
  Twiga Stars imeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo na Kocha Mkuu, Nasra Juma amesema vijana wake wote wapo katika hali nzuri na tayari kuwakabili Wazimbambwe.
  Aidha, Nasra amewaomba wapenzi wa soka nchini kujitokeza kwa wingi uwanjani Ijumaa kuwapa sapoti mabinti waweze kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
  Wakati huo huo: Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa ahadi kwa Twiga Stars, wakishinda mchezo huo kila mchezaji atapata Sh 300,000.
  Wambura amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau wa michezo wamekusanya shilingi milioni 15 ambazo zitatumika kama motisha kwa wachezaji hao.
  Aidha alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa michezo kuzidi kujitokeza na kuisaidia timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuhudhuria kwa wingi katika mchezo wa Machi 04, 2016 dhidi ya Zimbabwe utakayochezwa katika uwanja wa Chamazi.
  Aliongeza kuwa msaada zaidi unahitajika ili kuiwezesha timu hiyo kukidhi mahitaji yake muhimu,hivyo alitoa wito kwa wadau mbalimbali kutoa michango yao kupitia Twiga Special Fund, Akaunti na: 20110001677 iliyoko NMB tawi la Bank House jijjini Dar es Salaam.
  Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa ameipongeza Serikali kwa jitihada zake za kuhakikisha Twiga Stars inapata huduma muhimu ikiwemo motisha kwa wachezaji na benchi la ufundi.
  Mwesigwa pia amewapongeza wadau wote waliojitolea kusaidi timu hiyo ambapo amesema kujitokeza kwa wadau hao kunaongeza morali ya wachezaji.
  Msaada huo wa shilingi milioni 15 umetolewa na wadau watatu ambapo mmoja aliyechangia shilingi milioni 3 aliomba jina lake lihifadhiwe, wengine ni Kampuni ya ASAS shilingi milioni 2 na Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) shilingi milioni 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAHABESHI KUCHEZESHA MECHI YA TWIGA NA ZIMBABWE KUFUZU FAINALI ZA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top