• HABARI MPYA

  Tuesday, March 01, 2016

  BARTHEZ: UKUTA WA YANGA MAKIPA TUNAKULA KIPUPWE TU

  Na Adam Fungamwango, DAR ES SALAAM
  KIPA wa Yanga Ally Mustapha 'Barthez' amesema kuwa anafurahishwa na kazi inayofanywa na mabeki wa timu yake kiasi cha kuwaweka salama makipa wa timu hiyo.
  Barthez alisema hayo, baada ya kudaka mechi zote mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius bila kufungwa.
  Alisema kuwa kwa sasa makipa wa Yanga wako kwenye mikono salama mbele ya mabeki wa timu hiyo, ambao wamewafanya kujiamini zaidi.
  "Yaani nikwambie ndugu yangu, hakuna utofauti kati ya akicheza Kelvin (Yondani) na 'Cannavaro' (Nadir Haroub) wala hao waliocheza mechi dhidi ya Simba kina Pato (Ngonyani)," alisema.
  Ally Mustafa 'Barthez' amesema kwamba kwa ukuta uliopo Yanga makipa hawana mawazo

  Alisema kuwa wote wana aina moja ya uchezaji kiasi cha yeye kama kipa kutoona mapungufu yoyote yake.
  "Ushahidi unaona walivyocheza kina Yondani kwenye ligi, sisi ndiyo timu ambayo imefungwa magoli machache zaidi, na kila Pato na Bossou (Vicent) wamecheza mechi tatu, mbili za kimataifa na moja tulicheza na Simba, lakini hatukuruhusu goli, ina maana beki zote ziko sawasawa," alisema.
  Alisema kuwa timu yao ya Yanga inajivunia kwa hilo kwani si kila timu wakikosekana mabeki tegemeo inakuwa bado iko imara.
  "Kuna timu akikosena beki mmoja tu matatizo, lakini sisi tunapeta tu," alisema kipa huyo wa zamani wa timu za Mogo FC, Pentagon, Mkunguni, Ashanti na Simba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARTHEZ: UKUTA WA YANGA MAKIPA TUNAKULA KIPUPWE TU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top