• HABARI MPYA

    Tuesday, March 15, 2016

    TWIGA STARS KUONDOKA IJUMAA, TFF YADAI KUPAKAZIWA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    TIMU ya taifa ya soka ya wanawake, Twiga Stars inatarajiwa kusafiri siku ya Ijumaa kuelekea nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini Cameroon.
    Kikosi cha Twiga Stars kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa Karume chini ya kocha mkuu, Nasra Juma kujiandaa na mchezo huo muhimu ili kuweza kusonga mbele katika hatua inayofuata.
    Kuhusu maendeleo ya kambi, kocha Nasra Juma amesema vijana wake wanaendela vizuri, wamekua wakiendelea na mazoezi tangu baada ya mchezo wa awali na ana imani watafanya vizuri katika mchezo wa marudiano.
    Kiungo mshambuliaji tegemeo wa Twiga Stars, Mwanahamisi Omar 'Gaucho'

    Twiga Stars inahitaji ushindi katika mchezo huo wa marudiano utakaochezwa Jumapili, Machi 20 katika uwanja wa Rufalo uliopo jijini Harare ili kuweza kufuzu kwa hatua ya pili ya michuano hiyo.
    Wakati huo huo: Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesikitishwa na taarifa za upotoshaji za chombo kimoja cha habari ambacho mmoja wa watendaji alipata fursa ya kuhudhuria mkutano mkuu kama mgeni mwalikwa uliomalizika mwishoni mwa wiki jijini Tanga.
    "Katika hali inayotia mashaka, siku mbili kabla ya mkutano huo, chombo hicho kiliripoti kuwa wajumbe walikuwa wanalalamika kwa kutopelekewa nyaraka zinazohusiana na mkutano, wakati ukweli ni kuwa nyaraka hizo zilitumwa tangu mwezi Novemba 2015 zikiwa ni sehemu ya barua ya mwaliko wa kikao. Hivyo isingewezekana mwaliko wa kikao ukapokelewa na nyaraka zisiwepo. TFF inao ushahidi wa nyaraka hizo kuwafikia wajumbe wa mkutano huo.
    Katika toleo lake la leo chombo hicho kilidai TFF kupata hasara ya shilingi za kitanzania milioni 500.
    TFF inaviomba vyombo vya habari kuacha kupotosha juu ya taarifa za mkutano mkuu kuwa shirikisho lilipata hasara (loss) , TFF haifanyi biashara yoyote mpaka kufikia kupata hasara, kilichotokea ni kuongezeka kwa nakisi (deficit) katika bajeti ya mwaka 2014.
    Matumizi yaliongezeka kutokana na kulipa madeni ambayo uongozi wa sasa uliyakuta uliyosababisha hata basi la timu ya Taifa likamatwe, kuwepo kwa michezo mingi ya timu za Taifa (Taifa Stars, Twiga Stars, Serengeti Boys), gharama ambazo zilijumuisha kambi za maandalizi za timu pamoja na safari.
    Kwa kuwa TFF haifanyi biashara yoyote, matumizi yaliongezeka zaidi ya bajeti iliyokuwa imeratajiwa na kufanya kuwepo na upungufu wa zaidi ya milioni 490.
    Aidha TFF imesikitishwa na taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari mwishoni mwa wiki iliyopita, kuhusiana na suala la tiketi za Elektroniki.
    Ifahamike kwamba TFF ndiyo ilianzishwa matumumizi ya tiketi hizo kabla hazijasitishwa na Serikali mwaka jana kutokana na kubaini mapungufu katika utekelezaji.
    TFF haijawahi kugomea kuwepo kwa mfumo huo wa ki elektorniki, na kwa kushirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo wanaendelea na mazungumzo juu ya mfumo huo.
    Vikao vinaendelea kati ya Wizara na TFF ili kuona njia gani itaweza kutumika katika uendeshaji wa kuingia viwanjani kw aka kutumia mfumo wa ki elektroniki na kesho kutakuwepo na kikao Wizarani kujadili mradi huo.
    TFF inatafakari juu ya hatua za kuchukua dhidi ya wanaotoa taarifa za upotoshaji huo,"imesema taarifa ya TFF leo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TWIGA STARS KUONDOKA IJUMAA, TFF YADAI KUPAKAZIWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top