• HABARI MPYA

  Tuesday, March 15, 2016

  SHERMAN AITWA TIMU YA TAIFA YA LIBERIA

  KOCHA wa Liberia, James Debbah ameita amemjumuisha kwenye kikosi chake cha wachezaji 25, mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Kpah Sherman (pichani juu) anayechezea Santos ya Afrika Kusini kwa sasa
  Kwa ujumla, Debbah ameita wachezaji 19 wanaocheza nje katika kikosi hicho kwa ajili ya mchezo wa Kundi A kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 dhidi ya Djibouti baadaye mwezi huu.
  Debbah ameteua wachezaji watano tu wanaocheza nyumbani kwa ajili ya mechi mbili za nyumbani na ugenini dhidi ya Djibouti.
  Kikosi hicho kinaundwa na makipa; Tommy Songo (LISCR, Liberia), Samson Giddings (FC Fassell, Liberia), James Gally (Watanga FC, Liberia)
  Mabeki: Solomon Grimes (Nea Salamis Famagusta, Cyprus), Trokon Zeon (LPRC Oilers, Liberia), Gizzie Dorbor (HapoelAfula, Israel), Hilton Varney (Barrack Young Controllers, Liberia), Teah Dennis (Al-Ahli, Jordan), DirkirGlay (Mpumalanga Black Aces, South Africa), Omega Roberts (FK Donji Srem, Serbia), Alvin Macconough (Barrack Young Controllers, Liberia)
  Vioungo: Alseny Keita (Jeanne d’Arc de Drancy, Ufaransa), Dulee Johnson (Molde FK, Norway), Anthony Laffor (Mamelodi Sundowns, Afrika Kusini), Theo Weeks (Ermis Aradippou, Cyprus), Dioh Williams (Gefle IF, Sweden), Zah Kranga (FELDA United, Malaysia), Tonia Tisdell (Karabukspor, Turkey), Melvin George (Hantharwady United FC, Myanmar), Marcus Macauley (Al Ahli, Jordan).
  Washambuliaji: William Jebor (SD Ponferradina, Hispania), Sam Johnson (Djurgardens, Sweden),
  Patrick Wleh (Selangor FA, Malaysia), Sekou Conneh (Bethlehem Steel FC, Marekani) na Kpah Sherman (Santos, Afrika Kusini).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SHERMAN AITWA TIMU YA TAIFA YA LIBERIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top